CODERT kuwainua wazazi na vijana wa Mkoa wa Geita
Shirika la Misaada na Maendeleo ya Jamii (CODERT) limejipanga kuwasaidia jumla ya wananchi 7000 wanaoishi katika mazingira magumu Mkoani Geita ili waweze kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini linalowakabili.